Yanga kumshusha Chukwu Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2026
Yanga kumshusha Chukwu Dar

Wananchi wako busy sana kwenye dirisha hili la usajili. Yanga inafanya maboresho makubwa ya kikosi kwa lengo ya kujiimarisha baada ya misimu mitano mfululizo ya mafanikio.

Eneo la kiungo mkabaji ni miongoni mwa maeneo yaliyohitaji maboresho ambapo inaelezwa mchakato wa kuinasa saini ya nyota raia wa Nigeria Morrice Chukwu uko kwenye hatua za mwisho.

Chukwu ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba kunako klabu ya Singida BS. Matajiri hao kutoka mkoani Singida walikuwa kwenye mazungumzo nae ili kuhuisha mkataba wake lakini inaelezwa mazungumzo hayo yamevunjika baada ya Yanga kuingilia kati.

Unaweza kusema ni suala la muda sasa Chukwu atatua kwa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara akipishana na Mohamed Damaro ambaye amerejea Singida BS baada ya mkataba wake wa mkopo wa miezi 6 kumalizika.

Chukwu alikuwa mmoja wa wachezaji tegemea kwenye kikosi cha Singida BS katika misimu miwili iliyopita akimudu vyema kucheza kama kiungo mkabaji au beki wa kati.

Nyota hiyo alijiunga na Singida BS kwa mara ya kwanza akitokea klabu ya Rivers United ya Nigeria ambayo msimu wa 2022/23 ilichuana na Yanga robo fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC) ikifungwa mabao 2-0 huko Nigeria. Chukwu alikuwa sehemu ya kikosi hicho.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’