Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamekamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka klabu ya Mashujaa Fc, Hussein Juma Mihambo.
Yanga imekamilisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 19 wakimpa mkataba wa miaka minne.
Mihambo anatua kuongeza nguvu safu ya ushambuliaji akiwa ni mchezaji wa ndani.
Yanga inasukwa upya, usajili wa Mihambo ni sehemu ya maboresho eneo la ushambuliaji lakini pia mkakati wa kujenga kikosi kitakachotamba kwa muda mrefu.
Karibu Jangwani Mihambo..!
ADVERTISE HERE