Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa beki wa kulia Abdulnasir Gamal kutoka klabu ya Mashujaa FC.
Gamal anatua Yanga kuchukua nafasi ya Israel Mwenda ambaye Yanga imempa mkono wa kwaheri baada ya mkataba wake kumalizika.
Gamal alijiunga na Mashujaa msimu wa 2023-2024, akitokea Mlandege ya Zanzibar. Anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga katika dirisha hili akitokea Mashujaa Fc.
Mapema leo Yanga ilitambulisha usajili wa mshambuliaji kinda Hussein Juma Mihambo kutoka Mashujaa Fc.
Aidha Wananchi bado hawajamalizana na Mashujaa Fc, kama ilivyoripotiwa hapa wiki iliyopita, Wananchi pia wamemsajili beki wa kati Mohamed Mussa kutoka klabu hiyo ya Mashujaa.
Usajili wa Gamal na nyota wengine unalenga kuimarisha kikosi kwa ajili ya mafanikio ya muda mrefu.
Karibu Jangwani Gamal..!