Klabu ya Yanga inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo kinda Suleiman Mbarouk 'Mpemba D' kutoka visiwani Zanzibar.
Ni kiungo mahiri aliyekuwa akiitumikia JKU ambaye ana umri wa miaka 18 tu.
Ni usajili mwingine wa kimkakati unaofanywa na Yanga, kuongeza vipaji kwa ajili ya sasa na baadae.
Uhusiano mzuri kati ya Yanga na visiwa vya Zanzibar umeendelea kuwanufaisha mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwani kila mchezaji mwenye kipaji visiwani humo anatamani kuwatumikia wababe hao wa soka nchini.
Mpemba ataungana na nyota wengine kutoka visiwani Zanzibar waliosajliwa na Yanga katika dirisha hili Gamal na Mohamed Mussa ambao wametua wakitokea Mashujaa Fc.
Pale Jangwani wataungana na nyota wengine kutoka Zanzibar kama Ibrahim Bacca, Camemiro, Ninju na Mudathir Yahya