Yanga haitaacha kusajili wachezaji wazawa - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jul 2026
Yanga haitaacha kusajili wachezaji wazawa - Hersi

Rais wa Klabu ya Yanga SC, Injinia Hersi Said, amewatolea uvivu na kuwashukia vikali wadau wa soka wanaobeza usajili wa wachezaji wazawa uliofanywa na klabu hiyo, akitaja ukosoaji huo kama mtazamo hasi usio na tija kwa maendeleo ya soka la Kitanzania.

Akizungumza usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano maalumu wa klabu hiyo, Injinia Hersi amesema uongozi wa Yanga utakuwa wa "hovyo" kama utashindwa kuwapa fursa wachezaji wa ndani kuonyesha vipaji vyao kwenye timu kubwa.

"Mchezaji anayetoka timu nyingine ya hapa nyumbani, akija Yanga hata kwa msimu mmoja tu, kiwango chake hakiwezi kubaki pale pale. Thamani yake inaongezeka na kiwango kinakua kwa sababu ya mazingira na ushindani uliopo hapa," alisema Hersi kwa msisitizo.

Rais huyo aliongeza kuwa kelele na maneno ya kubeza usajili huo hayatawakatisha tamaa, na badala yake wataendelea kuwasajili na kuwakuza nyota wa ndani ili kulisaidia Taifa na timu ya taifa, Taifa Stars.

Katika dirisha hili la usajili kuelekea msimu mpya wa mashindano, Yanga imetambulisha rasmi wachezaji wazawa sita waliotua kwa mabingwa hao wa nchi.

Wachezaji hao ni:

  • Hussein Mihambo (Mshambuliaji – kutoka Mashujaa FC)
  • Juma Issa Abushiri (Winga – kutoka Fountain Gate)
  • Abdulnasir Muhamed (Beki wa pembeni – kutoka Mashujaa FC)
  • Mohamed Mussa (Beki wa kati – kutoka Mashujaa FC)
  • Erick Mwijage (Winga – kutoka KMC)
  • Suleiman Mbarouk "Mpemba D" (Kiungo – kutoka JKU ya Zanzibar)

Uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa mchanganyiko wa wachezaji hao sita wa ndani na nyota wapya wa kigeni waliosajiliwa, unalenga kutengeneza kikosi kipana kitakachopambana kutetea mataji ya ndani na kufika mbali zaidi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League).

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’