Pacome aondolewa kikosini 2026/27, Yanga kusajli mbadala wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jul 2026
Pacome aondolewa kikosini 2026/27, Yanga kusajli mbadala wake

Kutokana na changamoto ya majeraha inayomkabili kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametangaza rasmi kuwa profesa huyo wa mpira hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kuelekea msimu wa 2026/27 wakati akiendelea na matibabu.

Kamwe amesema tayari mchezaji huyo ameondolewa kwenye mfumo wa usajili 2026/27; lakini katika kipindi chote atakachokuwa nje, ataendelea kupata stahiki zake zote kama mchezaji wa Yanga.

Kamwe amesema Yanga itaongeza mchezaji mmoja wa kigeni ili kuziba nafasi ya kiungo mshambuliaji huyo ambaye aliumia Juni 30 katika mchezo wa mwisho ligi kuu ya NBC msimu uliopita dhidi ya JKT Tanzania.

Msemaji wa mabingwa hao wa nchi amebainisha kuwa sasa usajili wa nyota wa kigeni wamebaki wawili.

Kuhusu nyota wengine waliokuwa majeruhi Dickson Job na Clement Mzize, Kamwe amesema taarifa ya awali ilibainisha kuwa wachezaji hao wangerejea kikosini mwanzoni mwa Disemba 2026 lakini kutokana na kasi yao kwenye pre-season inayoendelea Avic Town, wanaweza kurejea mapema, pengine hadi mwezi Oktoba watakuwa tayari kucheza mechi za ushindani.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’