Kulingana na taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari Afrika Kusini, beki wa kati raia wa Ivory Coast Oumar Comara yuko mbioni kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga.
Comara anatokea klabu ya Golden Arrows ambayo msimu uliopita ilikuwa ikinolewa na kocha Manqoba Mngqithi ambaye sasa ni kocha mkuu wa Yanga.
Comara alikuwa miongoni mwa wachezaji wake tegemeo katika safu yake ya ulinzi Golden Arrows wakiwaliza nafasi ya sita PSL msimu uliopita.
Licha ya kucheza eneo la beki wa kati, Comara pia anamudu kucheza eneo la kiungo mkabaji hivyo ni mchezaji ambaye anaweza kutumika katika nafasi zote mbili.
Mwanahabari wa Afrika Kusini, Lorenz Kohler amedokeza kuwa tayari Yanga imekamilisha usajili wa beki huyo ambaye sasa anajiunga na kocha wake wa zamani.
Ujio wa beki huyo ni wazi unakwenda kukamilisha nyota wawili wa kigeni waliokuwa wamebaki Yanga pia ikihusishwa kumsajli kiungo mkabaji Fred Ngoma kutoka klabu ya OC Safi ya Morocco.
Lakini pia hatua hiyo inakwenda kufuta uwezekano wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kujiunga na Yanga kwenye dirisha hili.
Aidha Yanga pia italazimika kupunguza nyota mmoja wa kigeni taarifa za ndani zikidokeza kuwa mshambuliaji Laurindo Aurelio 'Depu' amewekwa sokoni.