Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema licha ya usajili mkubwa uliofanywa na klabu hiyo mpaka sasa, bado hawajamaliza.
Hersi amesema kuna usajili wa mchezaji mmoja 'funga kazi' ambao watautambulisha kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
"Tumefanya usajili mkubwa, hatutaki kurudia makosa ya msimu uliopita, nilikuwa sina amani nikiangalia mechi zetu. Nwahakikishie bado hatujafunga usajili."
"Kuna mchezaji mmoja tunakwenda kumtangaza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili," alisema Hersi
Wachezaji waliosajiliwa na Yanga kwenye dirisha hili mpaka sasa ni Cheikh Ibrahima TourΓ©, Housseine Zakouani, Albert Kangwanda, Peter Shalulile na Fred Ngoma.
Wengine ni Erick Mwijage, Juma Abushir, Suleiman Mbarouk. Mohamed Mussa na Abdulnassir Gamal na Hussein Mihambo
