Rais wa klabu ya Young Africans SC, Hersi Said, amewataka watu waliochukua Ngao ya Jamii 2025 kuirejesha, akisisitiza kuwa mataji ya soka yanapaswa kupatikana kwa ushindi wa uwanjani na si kwa njia nyingine yoyote.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama mapea leo, Hersi alisema tukio la kupotea kwa Ngao hiyo lilitokea wakati klabu hiyo ikiwa katika kipindi cha kusherehekea mafanikio yake.
βWakati tunasherekea ubingwa wetu, kuna watu wakaiba Ngao ya Jamii 2025. Kama kuna mtu analo alirudishe. Taji linashindaniwa uwanjani,β alisema Hersi.
Aliongeza kuwa Ngao hiyo ilitengenezwa nchini Tanzania, hivyo klabu hiyo tayari imechukua hatua ya kuagiza nyingine kutengenezwa.
βKwa bahati nzuri hii ilitengenezwa hapa hapa Tanzania, hivyo tumeagiza watutengenezee,β alisema.
Hersi pia alitoa wito wa moja kwa moja kwa waliohusika na kupotea kwa Ngao hiyo kuhakikisha wanairejesha, akisisitiza thamani ya ushindani wa haki katika mchezo wa soka.
βPia nichukue nafasi hii kuwaambia wale walioiba Ngao hii wairudishe. Rudisheni Ngao, taji hili linapatikana kwa kushinda uwanjani na sio kuiba,β alisema Hersi.
Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii 2025 wakiifunga Simba bao 1-0 katika mchezo uliopigwa Septemba 16 2025 uwanja wa Benjamin Mkapa.
