Droo hatua ya awali ligi ya mabingwa ni Alhamisi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Aug 2026
Droo hatua ya awali ligi ya mabingwa ni Alhamisi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetangaza kuwa droo ya hatua za awali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na Kombe la Shirikisho (CAFCC) kwa msimu wa 2026/2027 itafanyika Alhamisi ya tarehe 6 Agosti 2026.

Hafla hiyo kubwa inayofungua pazia la msimu mpya wa soka la klabu barani Afrika, itarushwa mubashara (LIVE) kutokea makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri.

Kupitia droo hiyo, klabu zote shiriki zitawafahamu wapinzani wao watakaokutana nao katika raundi ya kwanza ya kusaka tiketi ya kuingia hatua ya makundi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Idara ya Mashindano ya CAF, shughuli hiyo itaanza saa 8:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) kwa upande wa Kombe la Shirikisho, na kufuatiwa na droo ya Ligi ya Mabingwa itakayoanza saa 9:00 alasiri.

CAF imethibitisha kuwa baada ya droo hiyo kukamilika, timu zitakuwa na chini ya mwezi mmoja wa maandalizi kabla ya kushuka uwanjani. Michezo ya kwanza ya raundi ya awali imepangwa kuanza kuchezwa kati ya tarehe 4 hadi 6 Septemba 2026.

Baada ya hatua hiyo ya mchujo, michuano hiyo inatarajiwa kuingia hatua ya makundi kuanzia Novemba 27, 2026, hadi Januari 23, 2027. Hatua ya robo fainali na nusu fainali zitachezwa kati ya Februari na Aprili 2027, huku fainali kubwa za mashindano yote mawili zikitarajiwa kupigwa mwezi Mei 2027.

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wataiwakilisha nchi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa(CAFCL) pamoja na watani zao Simba huku Azam Fc na Singida BS zikishiriki kombe la Shrikisho (CAFCC).

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
38m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’