Jezi mpya za Yanga 2026/27 ni suala la muda tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Aug 2026
Jezi mpya za Yanga 2026/27 ni suala la muda tu

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema jezi mpya za mabingwa hao wa nchi kwa ajili ya msimu wa 2026/27 zitazinduliwa wakati wowote katika kipindi cha siku mbili.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari mapema leo, Kamwe alisema uzinduzi wa jezi hizo utakwenda sambamba na 'sapraizi' iliyoandaliwa kwa ajili ya Wananchi akiwataka mashabiki na wanachama wa Yanga kuwa tayari.

"Ndani ya siku mbili hizi kuanzia leo Jumatatu na kesho Jumanne, jezi ya msimu ujao ya Yanga itakwenda kuonekana. "

"Tunashindwa kusema ni wakati gani kwa kuwa kuna 'sapraizi' tutaifanya lakini muhimu jueni kuwa ndani ya siku izi mbili jezi ya Yanga itapatikana"

"Kwa wale ambao mnataka kununua andaeni fedha kabisa kwani ndani ya siku izi mbili tunakwenda kuzindua jezi bora ya muda wote ambayo haijawahi kutokea"

"Safari hii tumechukua mbunifu kutoka Ufaransa, hizi jezi mnazotuona tunavaa ni jezi za mazoezi sasa kama hizi ziko hivi je iyo jezi ya msimu?," alitamba Kamwe.

Aidha kuelekea wiki ya Mwananchi, uzinduzi utafanyika Ushirombo badala ya Katoro Geita palipotangazwa awali.

Kamwe amesema mabadiliko hayo yamezingatia umuhimu wa tukio hilo pamoja na ushiriki wa wadau wengine wakiwemo Azam TV ambao watarusha tukio hilo mbashara.

Wiki hii itakwenda sambamba na Yanga kushiriki uzinduzi wa uwanja Bukombe ambapo kikosi cha Yanga kitahusika ambapo wachezaji watapata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja huo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
17h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
21h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’