Shalulile kawatumia Simba salamu mapemaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Aug 2026
Shalulile kawatumia Simba salamu mapemaa

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga SC, usiku wa kuamkia leo walitambulisha usajili wa mshambuliaji hatari raia wa Namibia, Peter Shalulile, ambaye amefunguka kwa mara ya kwanza na kutuma salamu za mapema kwa watani zao wa jadi, Simba SC.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns ameeleza kuwa shauku yake kubwa ni kucheza mchezo wa watani wa jadi, maarufu kama 'Dabi ya Kariakoo'.

Shalulile amekiri kuwa dabi hiyo ina msisimko wa kipekee ambao umeanza kumgusa hata kabla hajakanyaga uwanjani.

"Kila ninapofikiria kuhusu mechi ya dabi, napata hisia za kipekee sana hadi nywele mwilini zinasimama. Kuna rafiki yangu anacheza Simba aliniambia kuwa hiyo ndiyo dabi bora zaidi utakayowahi kucheza maishani, na sasa nipo hapa kushuhudia wakati huo," alisema Shalulile kwa kujiamini.

Ujio wa mshambuliaji huyo unatarajiwa kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga, huku mashabiki wakitarajia kumuona uwanjani mapema tu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba uliopangwa kufanyika Agosti 12, 2026.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
30m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
48m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
54m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’