Yanga haikualikwa kukabidhiwa vifaa na wadhamini

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
4 Aug 2017
Yanga haikualikwa kukabidhiwa vifaa na wadhamini
Leo mchana kulikuwa na hafla maalumu ambapo wadhamini wa ligi, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ilikabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu inayodhaminiwa na kampuni hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 26.

Licha ya Yanga kuwa mabingwa watetezi, hawakupewa mwaliko rasmi na shirikisho la soka nchini (TFF) na hata Bodi ya ligi na hivyo kupelekea Yanga ikakosa mwakilishi kwenye hafla hiyo.

Hali hiyo ilipelekea Afisa Habari wa Simba, Haji Manara 'kujitolea' kuiwakilisha Yanga wakati vifaa vyake vilipotambulishwa.

Kitendo cha TFF kutotoa mwaliko kwa Yanga kimelaaniwa vikali na Katibu Mkuu, Charles Mkwasa.

Mkwasa amesema Yanga imesikitishwa na jambo hilo na hasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania, kwa kutoitendea haki Yanga.

"Hicho kitendo kimetusikitisha sana, kiuweli hali hiyo inatufanya tuonekane wazembe kwa mashabiki wetu kutokana na TFF ambao ndiyo waratibu," amesema Mkwasa.

"Niseme kuwa, TFF haijatupa mwaliko wa aina yoyote ikiwemo email (barua pepe), simu na hata kutufuata hapa ofisini kwetu maana siyo mbali kutoka hapo ofisini kwao.

"Kiukweli kitendo kimetusikitisha sana na kingine ninashangaa hao TFF hizo jezi zetu wamezitoa wapi? Kwa sababu hizo zilipelekwa kwa mmoja tuliyempa tenda ya kuziwekea logo, hiyo inamaana walipitia mlango wa nyuma na kutuzunguka kuchukua jezi bila ya kututaarifu washusika.

"Kitendo hicho huenda wenyewe TFF wakakiona kidogo lakini kwetu ni kikubwa na huenda kikaleta mpasuko klabuni kwetu,Ò€ amesisitiza Mkwasa

Ò€œKingine hao TFF kwanini wanapotukata makato yetu wanatoa taarifa, lakini hili la kukabidhiwa jezi wameshindwa kututaarifu?" amehoji.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
33m ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’