Yanga itafukuza mwizi kimyakimya - Tarimba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2018
Yanga itafukuza mwizi kimyakimya - Tarimba
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya klabu ya Yanga Abassi Tarimba amewataka wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa watulivu wakati Kamati hiyo ikitimiza majukumu.

Akizungumza jana baada ya swala ya Eid El Fitri, Tarimba amesema Kamati yake itashirikiana kikamilifu na Kamati nyingine za Yanga.

"Kamati yetu ni ya ushauri, imepewa majukumu maalum na Mkutano Mkuu wa Yanga. Kikubwa ambacho ningependa niwaambie WanaYanga, katika kipindi ambacho kama itakuwa inafanya kazi yake, tutakuwa makini sana" amesema Tarimba.

"Tutakuwa tunamfukuza mwizi kimyakimya. Hatutakuwa na kutangaza mara kwa mara miamala ambayo tutakuwa tunafanya"

"Miamala yote itakuwa ni siri yetu, sisi na Kamati ya Utendaji na vilevile tukishirikiana na Kamati ya usajili"

"Niwaombe Watanzania hasa wapenzi wa Yanga wakae kimya, wasubiri tufanye kazi ambayo tumepewa. Tunawaahidi, tutafanya kwa uadilifu na mapenzi ya hali ya juu."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
45m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’