Yanga inapambana kuongeza namba 10

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Aug 2026
Yanga inapambana kuongeza namba 10

Baada ya kushuhudia kilele cha wiki ya Mwananchi juzi, maoni ya wadau wengi yalimulika mapungufu eneo la kiungo cha ushambuliaji hasa mchezaji namba 10.

Kwenye dirisha hili Yanga haikusajili mchezaji namba 10 asilia na hivyo kubaki na Allain Okello pekee katika nafasi hiyo ambaye pia ianelezwa anawindwa na klabu moja barani Ulaya.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imebainisha kuwa kuna ofa inayofikia Bilioni 2 kwa ajili ya Okello na kama Yanga itafanikiwa kukamilisha sajili wanazozihitaji, pia wanaweza kumuuza Okello

Sasa inaelezwa mpango uliopo ni kuwa Yanga itasajili namba 10 nyingine ya boli kabla ya dirisha la usajili kufungwa na huenda asiwe mchezaji mmoja.

Baada ya kumkosa Stephane Aziz Ki ambaye imekuwa ngumu kuvunja mkataba wake na Al ittihad kutokana na masharti yaliyowekwa kwenye mkataba huo, Yanga ikarudisha majeshi kwa kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, Feisal Salum 'Fei Toto'.

Inaelezwa bado malengo ya Yanga kumpata Fei Toto yako palepale ingawa hawajafikia makubaliano na klabu yake ya Azam Fc juu ya dau la usajili.

Tetesi kutoka duru za usajili zimebainisha kuwa Yanga na Fei Toto tayari wana makubaliano binafsi na awali lengo lilikuwa kumtambulisha nyota huyo siku ya Jumapili kwenye Yanga Day lakini mpaka siku ya tukio makubaliano baina yao na Azam Fc yalikuwa hayajafikiwa.

Wamtupia macho Suleyman Fofana.

Inaelezwa pia Yanga imefungua mazungumzo na wasimamizi wa kiungo fundi wa Asec Mimosas Suleyman Fofana ili ajiunge na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.

Endapo watafikia makubaliano huenda Yanga ikatuma ofa Asec Mimosas kumsajili fundi huyo mahiri ili kuongeza nguvu safu yake ya kiungo cha ushambuliaji.

Aidha, mpango wa kumsajili kiungo wa Taifa Stars Alphonse Mabula haujazimika. Imeelezwa katika siku chache zilizobaki kuna sajili ya mchezaji mmoja au wawili inaweza kutambulishwa.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’