Zimbwe Jr amepania mchezo dhidi ya Simba Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Aug 2026
Zimbwe Jr amepania mchezo dhidi ya Simba Jumatano

Mlinzi wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba yamekamilika huku wachezaji wakipania kuanza vyema msimu kwa kutwaa Ngao ya Jamii.

Zimbwe Jr ambaye huu ni msimu wake wa pili tangu ajiunge na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara, amesema watakwenda kupambana kwa ari moja kwenye mchezo huo ili kuhakikisha wanashinda.

"Kwa niaba ya wachezaji wenzangu moja ya malengo yetu ni kuanza msimu vizuri kwa kushinda mechi hii muhimu ya kesho, naweza kusema tumejiandaa vizuri na sote tunafahamu umuhimu wa mchezo huu na tunatambua jukumu tulilonalo la kulinda na kulitetea taji letu."

"Tutaingia uwanjani tukiwa na umoja, ari na kujiamini tukiamini kwamba tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri"

"Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kesho, watusapoti na kuwa nyuma yetu katika kila dakika ya mchezo. Tunajua uwezo mkubwa wa kushangilia wa mashabiki wetu na tunahitaji sapoti yao ili kutupa nguvu zaidi ya kupambana hadi dakika ya mwisho," alisema Zimbwe Jr

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’