Yanga imetetea Ngao ya Jamii kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuichapa Simba bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Licha ya kuanza mchezo taratibu, Yanga ilirejesha umiliki baada ya dakika 25 na alikuwa ni Albert Kangwanda aliyefunga bao pekee la ushindi kwenye dakika ya 31 kwa kichwa akimalizia krosi ya Chadrack Boka.
Peter Shalulile almanusra aifungie Yanga bao la pili dakika chache baadae lakini shuti lake kutoka nje kidogo ya 18 likatoka nje sentimeta chache.
Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala mchezo kocha Manqoba Mngqithi akimuingiza Cheikh Toure na kumpeleka Shalulile upande wa winga wa kulia.
Yanga ilionekana kutengeneza mashambulizi ya hatari zaidi kuliko wapinzani wao lakini Simba walizinduka dakika 5 za mwisho wakijaribu kutafuta bao la kusawazisha.
Hata hivyo uimara wa mlinda lango Djigui Diarra na safu ya ulinzi kwa ujumla, walihakikisha lango linabaki salama na hatimaye kufanikisha ushindi wa Wananchi.
Ni taji la kwanza kwa Yanga msimu ukiwa ni mwanzo mzuri kwa mabingwa hao wa soka nchini wakiwa na mpango w akurejesha mataji yote Jangwani.



Wananchiiiiiiiiiiii...!