Yanayojiri Urusi : Nigeria nayo yapigwa, yafuata mkumbo wa Misri, Morocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Nigeria nayo yapigwa, yafuata mkumbo wa Misri, Morocco
Jana Nigeria ililazwa mabao 2-0 na Croatia hivyo kuungana na timu nyingine za Afrika zilizopoteza michezo ya kwanza, Morocco na Misri kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi.

Bao la kujifunga la Etebo na mkwaju wa penati wa Luka Modric uliihakikishia Croatia ushindi muhimu uliowapeleka kileleni kundi D ambalo pia linajumuisha timu za Iceland na Argentina.

Argentina ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Iceland katika mchezo wa mepama ambao mshambuliaji Lionel Messi alikosa mkwaju wa penati.

Nigeria ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye kundi hilo lakini kwa kipigo hicho, wana mazingira magumu kwani watalazimika kushinda michezo yao miwili iliyobaki dhidi ya Argentina na timu ngumu ya Iceland ili kufuzu kwa hatua ya mtoano.

Michuano hiyo inaendelea tena leo kwa michezo mitatu kupigwa.

mchezo wa mapema utapigwa saa tisa Alasiri kati ya Costa Rica dhidi ya Serbia halafu kufuatiwa na mchezo wa mabingwa watetezi, Ujerumani dhidi ya Mexico saa 12 jioni.

Brazil na Uswisi zitaumana kwenye mchezo wa mwisho siku ya leo utakaopigwa saa tatu usiku.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
21m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’