FT : Namungo Fc 1-3 Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Aug 2026
FT : Namungo Fc 1-3 Yanga, NBC PL

Yanga imeanza vyema kampeni ya kutetea taji la ligi kuu ya NBC kwa msimu wa sita mfululizo leo ikiichapa Namungo Fc mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Lindi.

Ulikuwa mchezo ambao Yanga ilitawala kwa muda mwingi ikitengeneza mashambulizi mengi huku wapinzani wao wakicheza kwa kujilinda zaidi na kutumia mashambulizi ya kushitukiza.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa suluhu ya bila kufungana licha ya Yanga kukosa nafasi kadhaa za wazi kupitia mshambuliaji wake kiongozi Peter Shalulile.

Yanga ilifanikiwa kufungua lango ya Namungo Fc dakika ya 68 kupitia kwa Chadrack Boka aliyemalizia mpira wa kona uliopigwa na Kangwanda.

Dakika nne baadae Maxi Nzengeli akaongeza bao la pili kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda lango.

Shambulizi kubwa Namungo Fc walifanya kwenye dakika ya 76 na kufunga bao pekee kupitia Helbert Lukindo.

Alikuwa ni Shalulile aliyefunga bao la tatu la Yanga dakika ya 89 akitumia makosa ya beki wa Namungo Fc Frank Magingi.

Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ugenini ambazo zimewasogeza hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’