Baada ya ushindi muhimu wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo Fc jana Wananchi wakianza vyema kampeni ya kutetea ubingwa kwa msimu wa sita mfululizo, kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo unaofuata.
August 20 Yanga itaikaribisha Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex.
Jana Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alitangaza rasmi kuwa msimu huu Yanga itacheza mechi zake za ligi nyumbani na kombe la CRDB katika uwanja wa KMC Complex badala ya uwanja wa Uhuru ambao awali walichagua kutumia.



ADVERTISE HERE