Miongoni mwa maeneo ambayo uongozi wa Yanga uliweka nguvu kubwa katika dirisha lililopita la usajili, ni safu ya ushambuliaji.
Mdhamini wa Yanga GSM ameweka 'pesa nyingi' katika eneo hilo ili kuhakikisha msimu huu hakuna timu itatoka salama.
Safu ya ushambilaji imesukwa upya wakisajiliwa Peter Shalulile, Cheick Ibrahima Toure na Selemani Mwalimu bila ya kumsahau kinda Hussein Mihambo ambaye kwa sasa atakuwa akipata uzoefu zaidi kutoka kwa miamba hao.
Lakini pia kama haitoshi, eneo la kiungo cha ushambuliaji pia limeongezwa nguvu na Stephane Aziz Ki, Albert Kangwanda na Hussein Zokouani ambao mapema tu wameonyesha thamani yao kikosini.
Ni wazi ushindani mkai unatarajiwa kushuhudiwa kwenye safu ya ushambuliaji kwani washambuliaji wote waliosajiliwa wana sifa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Wakati 'Sele Gomez' akitarajiwa kuanza kutumika kwenye mchezo ujao dhidi ya Coastal Union, Shalulile na Toure wameanza mapambano mapema.
Kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi alianza na Shalulile pale mbele hadi wakati wa mapumziko alipomuingiza Toure na Shalulile akasogea pembeni kuwa winga.

Mchezo dhidi ya Namungo Fc, Mngqithi akaanza na washambuliaji wote wawili lakini baada ya mapumziko akamtoa Toure.
Sele Gomez ameongezeka, akiwa na ari na morali kubwa ujio wake unampa Mngqithi machaguo zaidi kutegemea na mbinu anazotumia kwa kila mechi.
Baada ya kuwashuhudia Toure na Shalulile, Ni wazi mashabiki wa Yanga watatamani kumuona Mwalimu katika mchezo ujao pale uwanja wa KMC Complex