Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wako uwanja wa KMC Complex kuwakaribisha Coastal Union katika mchezo utakaopigwa saa 12:30 jioni.
Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Yanga leo itashuka uwanja wa KMC Complex ikiwa na lengo moja tu, kusaka ushindi ili kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi.
Utakuwa mchezo wa kwanza uwanja wa nyumbani, nafasi kwa mashabiki wa Yanga kuishuhudia timu yao kwa mara ya kwanza nyumbani msimu huu.
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi, Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amebainisha kuwa wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wao lakini wamejipanga kuhakikisha wanashiinda mchezo huo.
Huenda leo mashabiki wa Yanga wakashuhudia urejeo wa Stephane Aziz Ki ambaye Yanga imemsajili kutoka klabu ya Al Ittihad ya Libya.
Lakini pia inaweza ikawa nafasi kwa mashabiki kumshuhudia mshambuliaji Suleiman Mwalimu ambaye nae Yanga imemsajili kutoka klabua Wydad CA wakimn'goa kutoka mikononi mwa Simba.