Klabu ya Singida BS imethibitisha kuwasajili kiungo Mohamed Damaro 'Camara' na beki wa kulia Abdulnasir Mohamad 'Gamal' kutoka klabu ya Yanga.
Damaro amerejea katika klabu hiyo baada ya muda wake wa mkopo na Yanga kumalizika huku Gamal aliyejiunga na Wananchi kwenye usajili wa dirisha hili akitokea klabu ya Mashujaa Fc, amepelekwa kwa mkopo.
Singida BS inatajwa kukamilisha usajili huo siku ya mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa August 15, saa 5:59 usiku.
Damaro alitambulishwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kuelekea msimu huu na alishiriki mechi ya kilele cha wiki ya Mwananchi.
Hata hivyo benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Manqoba Mngqithi hakuwa na uhitaji na kiungo huyo baada ya usajili wa Fredy Ngoma
ADVERTISE HERE