Manqoba afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2026
Manqoba afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amesema mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania utakuwa mgumu pengine kuliko mechi zilizopita ambazo wamecheza mpaka sasa msimu huu.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Jumatatu kwenye uwanja wa KMC Complex, Manqoba amesema matokeo waliyopata JKT Tanzania kwenye mechi za mbili zilizopita hayaakisi ubora wao huku akimpongeza kocha Ahmed Ali kwa kazi nzuri aliyofanya.

"Kwa mtizamo wangu naona JKT Tanzania ni timu nzuri sana nafikiri matokeo waliyopata katika mechi zilizopita hayaakisi ubora wa timu yao. Kocha Ahmed Ali amefanya kazi nzuri."

"Wana wachezaji wengi wabunifu, ni timu inayoonekana kukua haraka, tunapaswa kwenda kuwakabili kwa umakini mkubwa," alisema Manqoba.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Manqoba alisema licha ya kutopata muda wa kutosha kujiandaa, vijana wake wako tayari kuendeleza mwanzo mzuri wa msimu huu.

Manqoba amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi ili kuendelea kuwapa hamasa wachezaji wake ambao ameahidi watapambana ili kuwapa furaha.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini amesema bado timu yake haijafika kwenye ubora anaohitaji kutokana na ufinyu wa muda wa maandalizi lakini anaamini kwa sapoti ya mashabiki, wachezaji watafanya zaidi na kuhakikisha wanashinda.

Manqoba amesema Yanga itaendelea kukosa huduma ya wachezaji wawili Dickson Job na Clement Mzize ambao ni majeruhi wa muda mrefu lakini wachezaji wengine wote wako tayari kwa mchezo huo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’