Yanga vs JKT Tanzania : Mshery awaita mashabiki KMC Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2026
Yanga vs JKT Tanzania : Mshery awaita mashabiki KMC Complex

Mlinda lango wa Yanga SC, Aboutwalib Mshery, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa KMC Complex kesho Jumatatu kuishangilia timu yao itakapokutana na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12:00 jioni, huku Yanga ikilenga kupata matokeo mazuri mbele ya JKT Tanzania katika mchezo ambao Mshery anaamini hautakuwa rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wao.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Mshery amesema kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi, licha ya ratiba kuwa na michezo inayofuatana kwa muda mfupi.

“Tunaendelea vyema na maandalizi ya michezo inayofuata mbeleni. Ukiangalia mechi zipo karibu sana, kila baada ya siku nne kuna mechi na maandalizi yanaendelea kama kawaida, lakini kwa sasa tumeweka nguvu zaidi kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania.”

Mshery amesema wanatambua ugumu wa mchezo huo kutokana na ubora wa JKT Tanzania, akisisitiza kuwa wapinzani wao wana wachezaji wazuri pamoja na benchi la ufundi lenye uwezo.

“Mchezo dhidi ya JKT Tanzania haujawahi kuwa mwepesi kwa sababu ni timu yenye wachezaji wazuri na mwalimu mzuri. JKT Tanzania wametoka kupoteza mchezo, hivyo tunajua watakuja kwa tahadhari zaidi.”

Kwa upande mwingine, mlinda lango huyo ametoa wito kwa mashabiki wa Yanga kujaza KMC Complex na kutoa sapoti kwa kikosi katika dakika zote za mchezo.

Mshery amesema uwepo wa mashabiki uwanjani ni sehemu muhimu ya kuwapa morali wachezaji wanapokuwa wakipambana kutafuta ushindi.

“Tunawaomba mashabiki wa Yanga kuja kutusapoti kama kawaida yao. Uwepo wao ni kama mchezaji wa 12 uwanjani, hivyo tunawaomba waje kwa wingi kuja kutupa sapoti.”

Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na lengo la kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, huku JKT Tanzania nayo ikitafuta matokeo yatakayoiweka katika nafasi nzuri zaidi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’