Chyna apewe maua yake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Aug 2026
Chyna apewe maua yake

Kuna kazi kubwa imefanywa na kocha wa viungo Tshepang 'Chyna' Mokaila katika msimu huu mpaka sasa.

Wakati wengi wakimsifu kocha Manqoba Mngqithi kwa mbinu zake ambazo mapema tu zimeanza kuwapa wakati mgumu timu pinzani, ni kwa sababu ana kundi la wachezaji ambao wameandaliwa kutekeleza mpango mkakati huo.

Katika mechi tatu za ligi kuu, Yanga imepachika mabao 11, huu ni uthibitisho ni kwa kiasi gani Yanga imewaacha mbali wapinzani wake.

Baada ya Manqoba kuteuliwa akapendekeza Mokaila aongezewe mkataba, wapo wachache 'hawakumuelewa' msimu uliopita lakini kile wanachoonyesha wachezaji sasa kinadhihirisha ule usemi kuwa changamoto iliyokuwa ikiitesa Yanga msimu uliopita ni uchovu zaidi kutokana na ufinyu wa kikosi.

Angalia kasi ya Yanga wanavyocheza wakiwa na mpira, lakini pia waangalie wanavyokimbia kuusaka mpira pale unapokuwa kwa wapinzani.

Kwa wastani Yanga imeweka umiliki wa mpira kwa asilimia 70, ikiwa ndio timu iliyoonyesha ubora mkubwa zaidi msimu huu.

Ni wazi wale waliokuwa na shaka na uwezo wa Mokaila sasa wamepata majibu kwa nini Yanga ilikubali kumuongezea mkataba baada ya pendekezo la kujumuishwa kwenye benchi la ufundi la Manqoba.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’