Yanga leo imeendeleza ubabe wake kwenye ligi kuu ya NBC ikiichapa Pamba Jiji mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Zilikuwa dakika 90 za moto kwa Pamba Jiji ambao watamshukuru mlinda lango wao kwa kuwanusuru kuondoka na kapu la mabao kwenye mchezo huo.
Yanga ilifunga mabao yote mawili kwenye kipindi cha kwanza, mshambuliaji Cheick Ibrahima Toure akitoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Maxi Nzengeli kabla ya yeye mwenyewe kufunga bao la pili akimalizia krosi ya Peter Shalulile.

Kulikuwa na nafasi kwa Yanga kufunga mabao zaidi hasa kipindi cha pili lakini uimara wa mlinda lango wa Pamba Jiji pamoja na kukosekana umakini kwa washambuliaji wa Yanga kuliwanyima Wananchi ushindi mnono.
Mshambuliaji Seleman Mwalimu aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Toure, angeweza kufungua akaunti yake ya mabao kama angetumia vyema nafasi mbili alizopata katika mchezo huo.
Ushindi huo umeirejesha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi wakiendelea kujipambanua kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga.