Ngoma ameanza kazi, awapa Wananchi matumaini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2026
Ngoma ameanza kazi, awapa Wananchi matumaini

Juzi mashabiki wa Yanga walimshuhudia kwa dakika 74 kiungo Fredy Ngoma akianza rasmi kutumika kwenye mechi za mashindano.

Ngoma raia wa Congo alijiunga na Yanga usajili wa dirisha lililopita akitokea Bizertin na alikuwa hajatumika kwenye mechi yoyote tangu msimu umeanza huku ikielezwa alikuwa bado hajawa fiti kuingia kwenye kikosi cha kocha Manqoba Mngqithi ambaye amekuwa akitaka mchezaji aliye fiti asilimia 100.

Katika mchezo huo ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, kwenye Uwanja wa KMC Complex kiungo huyo alionyesha kiwango cha juu akiwapa imani mashabiki wa Yanga ambao tangu kuondoka kwa Khalid Aucho, wanaamini pengo lake halikuwahi kupata mtu sahihi.

Katika mchezo huo, Ngoma alipiga jumla ya pasi 34 huku 32 zikifika wakati mbili zilipotea, lakini jambo bora zaidi kwake ni kwamba pasi zake nyingi ni zile za kwenda mbele.

Katika nafasi hiyo ni wazi atashirikiana na kiraka Duke Abuya ambaye unaweza kusema amemvutia zaidi Manqoba. Mara kadhaa kocha huyo raia wa Afrika Kusini amemsifu Abuya huku akibainisha kuwa ni mtu muhimu sana katika safu yake ya kiungo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’