Hatutawadharau Gaborone United - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Sep 2026
Hatutawadharau Gaborone United - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi cha Yanga kimejipanga kikamilifu kuhakikisha wanaanza vyema kampeni ya ligi ya mabingwa msimu huu.

Yanga iliwasili Botswana jana tayari kwa mchezo wa hatua ya awali mkondo wa kwanza dhidi ya Gaborone United utakaopigwa siku ya Jumamosi.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili nchini humo, Kamwe aliwahakikishia Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuwa timu yao iko imara na inakwenda kupambana ugenini kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ambayo yatawaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu raundi ya kwanza kwenye mchezo wa marudiano.

Kamwe amesema wanatambua ubora wa wapinzani wao na wanajua mchezo huo hautakuwa mwepesi.

"Timu imewasili salama hapa Gaborone, tumepata mapokezi mazuri, hapa kuna Watanzania wengi wanaishi. Lakini pia tuna sapoti kubwa ya mashabiki, wachezaji kama Peter Shalulile na Stephane Aziz Ki wanafahamika zaidi na mashabiki wa hapa"

"Sisi tumekuja kupambana ili tupate matokeo mazuri, tunatambua hakuna mchezo rahisi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ndio maana tumefanya usajili mkubwa ili kuhakikisha tunafanya vyema kwenye michuano hii," alisema Kamwe.

Baada ya kuwasili Botswana, vijana wa kocha Manqoba Mngqithi wameanza maandalizi kabambe kuelekea mchezo huo siku ya Jumamosi.

Mkakati wa Yanga ni kuanza na ushindi ugenini ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutinga raundi ya kwanza kwenye mchezo wa marudiano.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’