Yanga hakuna kulala FIFA Break, mazoezi kuendelea Avic Town

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2026
Yanga hakuna kulala FIFA Break, mazoezi kuendelea Avic Town

Kikosi cha Yanga leo kimerejea mazoezini wakijiandaa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya St George ya Ethiopia utakaopigwa kesho Ijumaa kwenye uwanja wa Uhuru.

Baada ya mchezo huo wachezaji walioitwa kwenye majukumu ya timu za Taifa wanatarajiwa kujiunga na mataifa yao kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2027 lakini kwa wale wengine watakaobaki, ni kazi kazi.

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi ameweka wazi mkakati wake wa kutumia kipindi hiki kuimarisha baadhi ya wachezaji ambao bado hawajafikia utimamu 'fitness' kwa asilimia 100.

Mara kadhaa Manqoba amefafanua sababu ya kutowatumia baadhi ya wachezaji au kuwatumia kwa dakika chache akieleza kutokuwa fit kwa asilimia 100.

β€œKatika kipindi cha mapumziko ya kalenda ya FIFA, tutakuwa na muda maalum wa kuwafanyia kazi wachezaji ambao bado hawajafikia kiwango kizuri cha utimamu wa mwili."

"Tutatumia kipindi hiki kuwapandisha hatua kwa hatua mpaka wafikie kiwango tunachokitaka,” alisema Mngqithi.

Wachezaji ambao Manqoba 'ana kazi nao' kwenye uwanja wa mazoezini ni pamoja na Dickson Job na Clement Mzize ambao wamekuwa nje kwa muda mrefu wakiwa majeruhi.

Lakini pia wamo Kibwana Shomari ambaye pia alikuwa majeruhi huku Stephane Aziz Ki naye akiingia kwenye kundi hilo baada ya kukosa sehemu kubwa ya maandalizi ya pre-season

Pia wamo wachezaji kama Fredy Ngoma na Farouk Komara ambao pia walichelewa kujiunga na wenzao kwenye pre-season.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
3h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’