Baada ya mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya St George ya Ethiopia ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, uongozi wa Yanga umewapa mapumziko wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa, nyota hao wamepewa mapumziko ya siku nane kabla ya kurejea kambini wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 10 kwenye uwanja wa Uhuru.
Ligi imesimama kwa takribani siku 21 kupisha kalenda ya FIFA ambapo bandika bandua ya ratiba itaendelea baada ya kukamilika kwa mechi hizo za Kimataifa zilizo ndani ya kalenda ya FIFA.
Pamoja na ligi kuu, mwezi Oktoba Yanga pia inakabiliwa mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA Fc ya Madagascar
ADVERTISE HERE