Yanga Princess yajiandaa kuikabili Simba Queens Ngao ya Jamii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Sep 2026
Yanga Princess yajiandaa kuikabili Simba Queens Ngao ya Jamii

Yanga Princess imeendelea na maandalizi kuelekea mchezo wake wa kwanza wa ushindani msimu huu, ambapo itakutana na watani wao wa jadi Simba Queens katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii ya Wanawake.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 30, utakuwa sehemu ya ufunguzi wa msimu mpya wa soka la Wanawake nchini na umebeba hamasa kubwa kutokana na historia ya ushindani kati ya timu hizo mbili za Kariakoo.

Uongozi wa Yanga umefanya maboresho makubwa kwenye kikosi cha Yanga Princess katika maandalizi ya msimu mpya, ikiwa ni sehemu ya kuongeza ushindani wa timu hiyo msimu huu.

Chini ya kocha Edna Lema, kikosi hicho kinaendelea na maandalizi katika uwanja wa KMC Complex, kikilenga kufungua msimu kwa matokeo mazuri dhidi ya Simba Queens.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, Septemba 30 kutakuwa na michezo miwili ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii.

Mchezo wa kwanza utawakutanisha JKT Queens na Mashujaa FC saa 9:00 alasiri, kabla ya macho yote kuelekezwa kwenye pambano la Kariakoo kati ya Yanga Princess na Simba Queens, litakalochezwa saa 12:00 jioni.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kamwe apongeza TFF kupima dawa za kusisimua miili
Kamwe apongeza TFF kupima dawa za kusisimua miili
1h ago
READ MORE β†’
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
5h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
21h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’