Tathmini ya mechi sita za mwanzo wa msimu Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2026
Tathmini ya mechi sita za mwanzo wa msimu Ligi Kuu

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga, wameanza kwa kasi msimu wa 2026/27, wakikusanya pointi zote 18 katika mechi sita za kwanza chini ya kocha wao, Manqoba Mngqithi.

Mngqithi, raia wa Afrika Kusini aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, ameanza kuonyesha athari ya kazi yake baada ya kikosi hicho kushinda michezo yote sita, huku kikifunga mabao 16 na kuruhusu mawili pekee.

Mwanzo huo umeifanya Yanga kuonekana kuwa imejipanga katika mbio za kutetea ubingwa, ingawa msimu bado ni mrefu na changamoto kubwa zaidi zinatarajiwa kujitokeza kadiri ratiba itakavyosonga.

Ligi imesimama kwa muda kutokana na kalenda ya FIFA ikitoa nafasi kwa timu kufanya tathmini ya mwenendo wa mwanzo wa msimu.

Safu ya ulinzi bado iko imara

Moja ya mambo yaliyojitokeza katika mwanzo wa msimu ni uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga.

Katika mechi sita, mabingwa hao wameruhusu mabao mawili pekee huku wakicheza mechi nne bila ya kuruhusu bao (ligi kuu).

Kipa Djigui Diarra pamoja na safu ya mabeki wamekuwa sehemu muhimu ya uimara huo, wakitoka na cleansheet kwenye mechi dhidi ya JKT Tanzania, Pamba Jiji, Fountain Gate na Geita Gold huku wakiruhusu bao kwenye michezo dhidi ya Namungo Fc na Coastal Union pekee.

Kwa timu inayolenga kutetea ubingwa, uwezo wa kupunguza mabao inayoruhusu ni sehemu muhimu ya kujenga matokeo ya muda mrefu.

Eneo la ushambuliaji limetoa mwanga

Yanga pia imeonyesha uwezo mkubwa katika eneo la ushambuliaji, ikiwa imefunga mabao 16 katika michezo sita.

Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Coastal Union na wa 4-0 dhidi ya JKT Tanzania ni miongoni mwa matokeo yaliyoonyesha uwezo wa timu hiyo kuzalisha mabao kwa wingi.

Hata hivyo, ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa mwisho kabla ya mapumziko umeonyesha kuwa si kila mchezo utakuwa rahisi kwa mabingwa hao.

Geita Gold ilitumia mfumo wa kujilinda kwa idadi kubwa ya wachezaji huku Yanga ikipata pigo kwa kiungo wake mshambuliaji Stephane Aziz Ki kutolewa nje kwa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza.

Mchezo huo ni wazi ulimpa mtihani wa kiufundi Mngqithi, hasa pale anapokutana na timu zinazokaa nyuma kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United

Mbali na uimara wa timu, kocha Mngqithi amedhihirisha kuwa kikosi chake kinaweza kushinda hata kinapowakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu.

Kadi nyekundu aliyopewa Stephane Aziz Ki katika mchezo uliopita iliwafanya Wananchi wacheze pungufu kwa zaidi ya dakika 75 na wakafanikiwa kufunga bao na kulind ushindi wao kwa dakika zote 90.

Ikumbukwe pia katika mchezo huo Manqoba alifanya 'rotation' kubwa ya kikosi akiwaweka nje baadhi ya wachezaji kama Peter Shalulile, Yao Kouassi, Chadrack Boka, Albert Kangwanda, nahodha Bakari Mwamnyeto wakiwa miongoni mwa wachezaji waliotumika kwenye mechi nyingi msimu huu.

Ni wazi licha ya mwanzo huo mzuri, Yanga bado ina safari ndefu katika kutetea taji lake. Mngqithi amepata mwanzo wenye matokeo mazuri, lakini michezo ijayo itakuwa kipimo muhimu cha uwezo wa timu kudumisha kiwango hicho dhidi ya wapinzani wenye mbinu tofauti.

Kwa sasa, mabingwa hao wameweka alama ya mwanzo kwa kushinda mechi zote sita na kukaa kileleni mwa msimamo.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini Septemba 28 kuendelea na maandalizi ya mechi zinazofuata ambapo Oktoba 10 Wananchi watawakabili watani zao Simba katika mchezo wa raundi ya 7 ligi kuu ya NBC.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
3h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’