Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye alikuwa mapumziko kwao nchini Ufaransa anatarajiwa kutua keshokutwa Jumamosi, tayari kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi na michuano ya Kimataifa.
Yanga itaanza kujifua Jumatatu, Juni 25 2018 ikiwa na kikosi kitakachojumuisha wachezaji wapya waliosajiliwa na wale ambao Zahera amehitaji 'kuwajaribu' kabla hajaidhinisha usajili wao.
Kulingana na mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, klabu hiyo imefanikiwa kuwasainisha mikataba mipya wachezaji wake waandamizi ambao mikataba yao ilikuwa imemalizika.
Mshambuliaji Obrey Chirwa ndiye mchezaji pekee miongoni mwa waliomaliza mikataba ambaye hajasaini na kuna taarifa tayari amesajiliwa na Ismailia ya Misri.
Wakati wowote Yanga itaweka hadharani orodha ya wachezaji ambayo tayari imewasajili pia wale ambao hawatakuwa na timu hiyo msimu ujao.
Kocha Mkuu wa Yanga Zahera, ametaka zoezi la usajili kwa wachezaji wa ndani liwe limekamilika kabla ya kuanza mazoezi Juni 25.

ADVERTISE HERE