Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema amekanusha uvumi unaoendelea kwenye kurasa za mitandao ya kijamii unaodai kuwa amejiuzulu nafasi yake kufuatia kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Simba Queens hapo jana kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii.
Kipigo hicho kiliwakera mashabiki wa Yanga ambao kwa muda mrefu wameishuhudia timu yao ikipoteza kila inapokutana na Simkba Queens na kupelekea kuibuka minong'ono mingi mitandaoni.
Edna amesisitiza kuwa yeye bado ni kocha wa Yanga Princess na hakujiuzulu kama ainavyoelezwa.
"Mimi bado ni kocha wa Yanga Princess na ninaendelea na majukumu yangu. Habari hizo ni uvumi tu ambao hauna ukweli wowote, " alisema Edna maarufu 'Mourinho'.
Baada ya kutupwa nje ya michuano ya Ngao ya Jamii, Yanga Princess inarejea uwanja wa mazoezi kukamilisha maandalizi kabla ya kuanza kwa mikiki mikiki ya ligi kuu ya Wanawake 2026/27
Jumamosi Yanga Princess itakamalisha mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Mashujaa Queens