TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewaruhusu wachezaji wa Yanga SC, Simba SC na Singida Black Stars waliopo kwenye kambi ya Taifa Stars kurejea katika klabu zao kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao, ikiwemo Dabi ya Kariakoo.

Hatua hiyo imekuja baada ya klabu hizo kuwasilisha maombi ya kuwarudisha wachezaji wao kutoka kwenye kambi ya Taifa Stars.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Evans Mgeusa, amekanusha taarifa inayodai wachezaji wa Yanga pekee ndio wameruhusiwa kwani si Yanga SC pekee iliyowasilisha ombi la kurejesha wachezaji wake, bali pia Simba SC na Singida Black Stars wameomba wachezaji wao kurejea kwenye klabu.

Mgeusa amesema maombi yote yamekubaliwa na TFF, huku Yanga SC ikiwa imewasilisha ombi hilo mapema zaidi.

β€œYanga SC wao waliomba tangu Septemba 30, 2026, ila Simba SC na Singida Black Stars wao wameomba jana, Oktoba 1, 2026, na wote tumewaruhusu,” alisema Mgeusa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, wachezaji wa Yanga SC wanatarajiwa kuondoka kambini kesho, huku Simba SC na Singida Black Stars zikiwa bado hazijakata tiketi za safari za kuwarejesha wachezaji wao nchini.

β€œWachezaji wa Yanga SC wanaondoka kesho, hao ndio najua. Ila Simba SC na Singida BS bado timu zao hazijakata tiketi ili tujue ni lini wanaondoka kambini kurudi Tanzania,” aliongeza Mgeusa.

Timu ya Taifa iko nchini Morocco kucheza mechi za kirafiki baada ya kukamilika kwa mechi mbili za kuwania kufuzu Afcon 2027.

Oktoba 05 Stars itachuana na wenyeji wao Morocco

Nyota wa Yanga walio kwenye kikosi cha Stars ni Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya na Seleman Mwalimu baada ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto kushindwa kusafiri kutokana na changamoto za kifamilia

Yanga SC Stories

Badru afichua Kazimoto kupandishwa kikosi cha kwanza
Badru afichua Kazimoto kupandishwa kikosi cha kwanza
4h ago
READ MORE β†’
Chuga Boy aongezwa kikosi cha Stars U23
Chuga Boy aongezwa kikosi cha Stars U23
7h ago
READ MORE β†’
Dabi ya Kariakoo kupigwa dimba la Uhuru
Dabi ya Kariakoo kupigwa dimba la Uhuru
9h ago
READ MORE β†’
Hizi hapa mechi za Yanga Oktoba
Hizi hapa mechi za Yanga Oktoba
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 02 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 02 2026
15h ago
READ MORE β†’
Siku ya tatu ya maandalizi KMC Complex
Siku ya tatu ya maandalizi KMC Complex
1d ago
READ MORE β†’
Edna Lema akanusha kujiuzulu Yanga Princess
Edna Lema akanusha kujiuzulu Yanga Princess
1d ago
READ MORE β†’
Mngqithi awaangazia vijana wanaogombea nafasi Yanga
Mngqithi awaangazia vijana wanaogombea nafasi Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Kutofautiana uwanjani ni kawaida - Mwamnyeto
Kutofautiana uwanjani ni kawaida - Mwamnyeto
1d ago
READ MORE β†’
Dozi yao iinaandaliwa kimyakimya
Dozi yao iinaandaliwa kimyakimya
1d ago
READ MORE β†’