TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2026
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewaruhusu wachezaji wa Yanga SC, Simba SC na Singida Black Stars waliopo kwenye kambi ya Taifa Stars kurejea katika klabu zao kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao, ikiwemo Dabi ya Kariakoo.

Hatua hiyo imekuja baada ya klabu hizo kuwasilisha maombi ya kuwarudisha wachezaji wao kutoka kwenye kambi ya Taifa Stars.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Evans Mgeusa, amekanusha taarifa inayodai wachezaji wa Yanga pekee ndio wameruhusiwa kwani si Yanga SC pekee iliyowasilisha ombi la kurejesha wachezaji wake, bali pia Simba SC na Singida Black Stars wameomba wachezaji wao kurejea kwenye klabu.

Mgeusa amesema maombi yote yamekubaliwa na TFF, huku Yanga SC ikiwa imewasilisha ombi hilo mapema zaidi.

β€œYanga SC wao waliomba tangu Septemba 30, 2026, ila Simba SC na Singida Black Stars wao wameomba jana, Oktoba 1, 2026, na wote tumewaruhusu,” alisema Mgeusa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, wachezaji wa Yanga SC wanatarajiwa kuondoka kambini leo, huku Simba SC na Singida Black Stars zikiwa bado hazijakata tiketi za safari za kuwarejesha wachezaji wao nchini.

β€œWachezaji wa Yanga SC wanaondoka kesho (leo), hao ndio najua. Ila Simba SC na Singida BS bado timu zao hazijakata tiketi ili tujue ni lini wanaondoka kambini kurudi Tanzania,” aliongeza Mgeusa.

Timu ya Taifa iko nchini Morocco kucheza mechi za kirafiki baada ya kukamilika kwa mechi mbili za kuwania kufuzu Afcon 2027.

Oktoba 05 Stars itachuana na wenyeji wao Morocco

Nyota wa Yanga walio kwenye kikosi cha Stars ni Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya na Seleman Mwalimu baada ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto kushindwa kusafiri kutokana na changamoto za kifamilia

Yanga SC Stories

Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
14h ago
READ MORE β†’
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awaaga Wananchi
Dladla awaaga Wananchi
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’