Kariakoo Derby: TFF yajizatiti kudhibiti matukio vyumba vya kubadilishia nguo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Kariakoo Derby: TFF yajizatiti kudhibiti matukio vyumba vya kubadilishia nguo

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Cornel Barnabas, amesema maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga utakaofanyika Oktoba 10 yamehusisha hatua mpya za kiusalama, ikiwemo matumizi ya kifaa maalum cha kugundua harufu katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Cornel amesema kifaa hicho kitatumika katika mchezo huo wa Derby ya Kariakoo ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa kuhakikisha mazingira ya mchezo yanakuwa salama na yanazingatia taratibu zinazotakiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya TFF jijini Dar es Salaam, Cornel amesema kifaa hicho hakitatumika kwenye Kariakoo Derby pekee, bali kitaendelea kutumika pia katika michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu zinapokuja mechi hizo ambapo mara kadhaa hasa klabu ya Yanga imegoma kuingia kwenye vyumba kutokana hofu ya uwepo wa dawa za kuwapunguza nguvu wachezaji.

FVS itatumika, TFF yaweka masharti

Katika hatua nyingine, Cornel, amesema makocha wa Simba na Yanga watapewa kadi mbili katika mchezo huo ambazo zitatumika kuomba review ya matukio kupitia mfumo wa FIFA Video Support (FVS).

Cornel amesema utaratibu huo ni sehemu ya hatua mpya za matumizi ya teknolojia katika kusimamia mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, huku makocha wakipewa nafasi ya kuomba mapitio ya matukio wanayoona yanahitaji kuchunguzwa zaidi.

"Kwenye mechi kutakuwa na Kadi nne za kuomba FVS itumike , Kila benchi litapewa hizi kadi mbili , linapotokea tukio ambalo benchi linahitaji msaada wa FVS ili haki itendeke litaonesha kadi juu na refa ataenda kwenye FVS. Sharti ni kwamba benchi linatakiwa kuonesha kadi yao juu ndani ya sekunde 60 haitakiwi kuchelewa hadi tukio lipite," alisema

Cornel amesema mfumo huo hautatumika kwenye Kariakoo Derby pekee, bali kadi hizo zitatumika pia katika michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mechi ya mkondo wa kwanza CFFA vs Yanga itapigwa Mauritius
Mechi ya mkondo wa kwanza CFFA vs Yanga itapigwa Mauritius
5h ago
READ MORE β†’
Anayetaka kujua ubora wa Yanga aje uwanjani Jumamosi - Samwel
Anayetaka kujua ubora wa Yanga aje uwanjani Jumamosi - Samwel
6h ago
READ MORE β†’
Abuya kuhitimisha majukumu ya Kimataifa leo
Abuya kuhitimisha majukumu ya Kimataifa leo
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 05 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 05 2026
9h ago
READ MORE β†’
Doumbia amepata chimbo jipya Morocco
Doumbia amepata chimbo jipya Morocco
22h ago
READ MORE β†’
BBD yuko tayari kuendeleza alipoishia
BBD yuko tayari kuendeleza alipoishia
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 04 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 04 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga Princess mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
Yanga Princess mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yajipima na JKT Tanzania Gymkhana
Yanga yajipima na JKT Tanzania Gymkhana
2d ago
READ MORE β†’
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea
2d ago
READ MORE β†’