Kiungo kiraka wa Yanga Maxi Nzengeli Jumamosi atakuwa akiisaka rekodi kwenye mchezo wa Kariakoo Derby wakati Simba watakapokuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa uwanja wa Uhuru.
Maxi ni miongoni mwa wachezaji wanaoongoza kwa kufunga mabao mengi kwenye mchezo huo wa Kariakoo Derby.
Kama atafunga kwenye mchezo unaofuata, basi atajipambanua kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kihistoria katika mechi za Simba na Yanga karne ya 21.
Maxi amefunga mabao matatu katika mechi dhidi ya Simba akiwa sawa na Stephane Aziz Ki. Hata hivyo Aziz Ki anatumikia adhabu ya kadi nyekundu hivyo atakosa mchezo huo.
Msimu huu Maxi amekuwa kwenye kiwango bora akicheza mechi zote sita za Yanga kwenye ligi akifunga mabao matatu na kutoa asisti moja.
Katika mechi hizo sita, mechi tano aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo.
Nyota huyo wa Kimataifa kutoka DR Congo anahitaji kufunga bao moja tu ili jina lake lijipambanue katika rekodi za Kariakoo Derby.