Boka, Yao tayari kwa kazi maalum dabi ya Kariakoo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Boka, Yao tayari kwa kazi maalum dabi ya Kariakoo

Mashabiki wa Yanga wanahesabu saa kabla ya kuelekea uwanja wa Uhuru kushuhudia mchezo wa dabi ya Kariakoo wakati timu yao itakapokuwa ikimenyana na Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Mtanange huo wa kukata na shoka unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 1 usiku, Yanga wakiwa ugenini.

Yanga inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa katika nyakati nzuri kwani wachezaji wote wako tayari.

Mkufunzi wa Yanga Manqoba Mngqithi amekiandaa kikosi chake kikamilifu akiahidi kuwadhiiti Simba katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyatumia kufunga mabao.

Manqoba alisema timu hiyo imekuwa ikitumia zaidi mipira iliyokufa kufunga mabao ambapo kati ya mabao 11, mabao 7 wamefunga kupitia aina hiyo ya mpira.

Mawinga wao Anicet Oura na Libasse Gueye ndio wanaonekana kuhusika zaidi kwenye kusababisha mabao hayo hasa Libasse ambaye amehusika kwenye mabao 6 yaliyofungwa na timu hiyo.

Manqoba amewaandaa walinzi wake wa pembeni Yao Kouassi na Chadrack Boka kuhakikisha hakuna madhara yanayosababishwa na wachezaji hao kwenye maeneo yao.

Yao na Boka wamethibitisha kwenye mechi zilizopita dhidi ya Simba wakifanikiwa kuwadhibiti wachezaji hao wa pembeni, leo watahitaji kufanya tena jukumu hilo kwa ufanisi.

Lakini pia eneo la ushambuliaji la Yanga linalotarajiwa kuongozwa na Peter Shalulile linapaswa kuwa na ukatili kwa kutumia nafasi zitakazotengenezwa.

Manqoba amesema hana wasiwasi na utengenezaji wa nafasi kwenye kikosi chake, amekuwa akifanya kazi kwenye uwanja wa mazoezi ili kuwaongezea washambuliaji wake ufanisi kwenye matumizi ya nafasi hizo.

Amesema ipo siku kuna timu italipa gharama ya idadi ya nafasi ambazo wamekuwa wakizipoteza, anaamini siku hiyo timu yake itafunga mabao mengi.

Je siku hiyo inaweza kuwa leo? Itafahamika pale uwanja wa Uhuru saaa 1 usiku...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
Matchday; Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
3h ago
READ MORE β†’
Vifaa maalumu vya kupima ubora wa hewa vitawekwa vyumbani
Vifaa maalumu vya kupima ubora wa hewa vitawekwa vyumbani
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 10 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 10 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi yampa jeuri Manqoba, apania ushindi dhidi ya Simba
Maandalizi yampa jeuri Manqoba, apania ushindi dhidi ya Simba
20h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka mkakati wa kuidhibiti Simba Kariakoo Derby
Manqoba aweka mkakati wa kuidhibiti Simba Kariakoo Derby
23h ago
READ MORE β†’
Ni Arajiga tena Kariakoo Derby
Ni Arajiga tena Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Kimya kingi kina mshindo mkuu
Kimya kingi kina mshindo mkuu
1d ago
READ MORE β†’
Iweke Xtra 90 katika simu yako
Iweke Xtra 90 katika simu yako
1d ago
READ MORE β†’
Hivi hapa viingilio Dabi ya Kariakoo Jumamosi
Hivi hapa viingilio Dabi ya Kariakoo Jumamosi
1d ago
READ MORE β†’
CFFA kutumia dimba la Azam Complex mechi dhidi ya Yanga
CFFA kutumia dimba la Azam Complex mechi dhidi ya Yanga
1d ago
READ MORE β†’