FT : Simba 2-1 Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
FT : Simba 2-1 Yanga, NBC PL

Yanga imepoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba leo ikikubali kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru.

Peter Shalulile aliitanguliza Yanga mapema kwa bao la dakika ya tano akimalizia pasi ya Maxi Nzengeli.

Hata hivyo unaweza kusema mpango wa kocha Manqoba Mngqithi leo haukufanya kazi mbele ya Simba waliotawala mchezo kwa muda mwingi na kulazimu Yanga wajilinde kwa muda mwingi.

Aidha kuumia kwa Duke Abuya mapema kwenye kipindi cha kwanza unaweza kusema kulivuruga mpango wa timu, Simba wakionekana kutawala eneo la kiungo.

Kipindi cha pili hakikuwa na mabadiliko makubwa upande wa Yanga wakibaki nyuma kwa muda mwingi na kuwaruhusu Simba kutawala mchezo.

Neo Maema akaifungia Simba bao la kusawazisha kabla ya Elie Mpanzu kufunga bao la pili dakika nne baadae.

Ni mchezo ambao unaweza kusema wachezaji wa Yanga wanapaswa kusahau haraka kwani hawakuwa katoka ubora uliotarajiwa.

Yanga ina siku tatu kabla ya mchezo mwingine dhidi ya TRA United utakaopigwa Oktoba 13 dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Ni matokeo ya mpira wa miguu, ziko nyakati za furaha lakini zipo nyakati za furaha kwa mpinzani wako.

Leo ni furaha kwa Simba hasa ikizingatiwa kabla ya mchezo huu walicheza misimu minne bila ya kupata ushindi dhidi ya Yanga kwenye ligi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Bado tuna mechi 23 msimu huu - Kamwe
Bado tuna mechi 23 msimu huu - Kamwe
10m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
Kikosi : Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
4h ago
READ MORE β†’
Boka, Yao tayari kwa kazi maalum dabi ya Kariakoo
Boka, Yao tayari kwa kazi maalum dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
Matchday; Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
12h ago
READ MORE β†’
Vifaa maalumu vya kupima ubora wa hewa vitawekwa vyumbani
Vifaa maalumu vya kupima ubora wa hewa vitawekwa vyumbani
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 10 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 10 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi yampa jeuri Manqoba, apania ushindi dhidi ya Simba
Maandalizi yampa jeuri Manqoba, apania ushindi dhidi ya Simba
1d ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka mkakati wa kuidhibiti Simba Kariakoo Derby
Manqoba aweka mkakati wa kuidhibiti Simba Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Ni Arajiga tena Kariakoo Derby
Ni Arajiga tena Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Kimya kingi kina mshindo mkuu
Kimya kingi kina mshindo mkuu
1d ago
READ MORE β†’