Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema haikuwa malengo yao kupoteza mchezo dhidi ya Simba lakini wamekubali kwa kuwa ni matokeo ya mpira wa miguu.
Kamwe amewataka Wanayanga kuwapa nafasi benchi la ufundi kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana kwa kuwa ndani ya siku chache wanakabiliwa na mechi muhimu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;
"Imewachukua Kolo Miaka mitatu na miezi mitano kupata Ushindi wa kwanza kwenye Ligi mbele yetu .. Thatβs Football na FAIR PLAY kwao kwa Dakika 90 nzuri
Tusingeweza kushinda kila siku, Kila mechi ya Derby .. Haiwezekani, Unless umejua mpira kupitia TikTok.
Ukiangalia Msimamo wa Ligi kwa sasa utaona bado mechi 23 mbele.. Ligi Bado mbichi hii. Kuna Pointi nyingi za kugombea
Na aliye kileleni ni hiyo Baiskeli ya Miti.. ni JUKUMU LETU sasa kama YANGA kuweka nguvu na kurudi Kileleni.. Na Linawezekana kabisa. Hizo ndio shughuli zetu za kila siku wala aina shaka Yeyote
Kwa sasa Tujiweke sawa kwenye CHAMPIONS LEAGUE. Tuwape muda Benchi la Ufundi na Players wetu waende kwenye Uwanja wa mazoezi kutafuta majibu ya maswali tuliyokosea Leo..
Kuna mechi ya kutafuta Tiketi ya Group Stage Jumamosi.. Hii ni Muhimu sana kwa maana Tukikosea hapo Maumivu yake Yatakuwa makali sana sana zaidi ya Leo
Daima Mbele Wanangu .. atakayecheka mwisho wa Msimu ndio atakayecheka vizuri"