Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya TRA United dhidi ya Yanga uliopangwa kupigwa Oktoba 13, umepigwa kalenda.
Yanga ilipaswa kusafiri kuelekea mkoani Arusha kwa ajili ya mchezo huo kabla ya kuhamisha nguvu kwenye ligi ya mabingwa.
Baada ya mchezo huo kupigwa kalenda, Yanga sasa inaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA ya Madagascar.
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Oktoba 17 kwenye uwanja wa Azam Complex.
ADVERTISE HERE