Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2026
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amesema klabu hiyo inaweka mkazo katika maandalizi ya kiakili na kiufundi kuelekea michezo miwili dhidi ya CFFA ya Madagascar, katika hatua ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akisisitiza kuwa hawapaswi kuruhusu kipigo cha Simba kuathiri safari yao ya kimataifa.

Yanga inatarajiwa kukutana na CFFA Jumamosi, Oktoba 17, kabla ya kurudiana Jumatano, Oktoba 21, huku michezo yote miwili ikipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani, Kamwe amesema maandalizi ya timu yanahitaji umakini mkubwa, hususan katika eneo la kisaikolojia, baada ya kupoteza mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba kwa mabao 2-1.

Amesema matokeo ya mchezo huo yanapaswa kuwa funzo kwa kikosi hicho badala ya kuwa kikwazo katika maandalizi ya kukabiliana na wapinzani wao wa kimataifa.

Kamwe amebainisha kuwa timu pinzani katika mashindano ya Afrika hufuatilia kwa karibu matokeo ya wapinzani wao, hali ya wachezaji na mazingira yanayoweza kuwapa nafasi ya kupata matokeo mazuri.

“Unapotoka kucheza derby na kupoteza, halafu unakutana na mchezo muhimu wa CAF Champions League, unahitaji kuwa makini zaidi katika maandalizi yako, hasa katika eneo la kisaikolojia,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa Yanga haipaswi kuruhusu changamoto iliyotokana na kipigo cha Simba itumike na CFFA kama fursa ya kuipata katika mazingira magumu, akiwataka wachezaji kurejesha umakini na kuelekeza nguvu zao katika malengo ya klabu.

Katika hatua nyingine, Kamwe amesema michezo hiyo miwili itachezwa nchini Tanzania kwa utaratibu uliokubaliwa na pande husika, licha ya mchezo wa kwanza wa Oktoba 17 kuwa wa CFFA kwa mujibu wa upangaji wa ratiba.

Hali hiyo inaifanya Yanga kucheza mechi zote mbili katika Uwanja wa Azam Complex, jambo linaloipa timu hiyo fursa ya kutumia mazingira inayoyafahamu, ingawa Kamwe amesisitiza umuhimu wa maandalizi makini na kutowadharau wapinzani wao.

Aidha, uongozi wa Yanga umewataka mashabiki na wanachama kuendelea kuiunga mkono timu katika kipindi hicho muhimu, huku klabu ikielekeza nguvu zake katika kutafuta matokeo yatakayoiwezesha kusonga mbele katika mashindano hayo ya kimataifa.

Yanga SC Stories

Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
9h ago
READ MORE β†’
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
10h ago
READ MORE β†’
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
12h ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
1d ago
READ MORE β†’
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga ilivyojifua New Amaan Complex, Zanzibar
Yanga ilivyojifua New Amaan Complex, Zanzibar
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’