FT : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL R1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
FT : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL R1

Dakika 90 za mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa (CAFCL) zimemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0.

Wananchi wameandikisha ushindi muhimu ambao unawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi sasa wakihitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare na kutopoteza kwa zaidi ya mabao manne kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 21 kwenye uwanja wa Azam Complex.

Ni sahihi kusema ni muujiza pekee ambao utawafanya Wananchi wasifuzu makundi kwa kuzingatia kile walichoonyesha kwenye mchezo huo.

Ulikuwa mchezo ambao pengine Yanga ilistahili kuondoka na ushindi mnono zaidi kwa kuzingatia idadi ya nafasi walizotengeneza hasa kipindi cha kwanza.

Alikuwa ni Ibrahim Toure aliyefunga bao la kwanza kwenye dakika ya 42 akitumia makosa ya mlinda lango wa CFFA.

Kipindi cha pili Yanga waliendelea kupeleka presha langoni kwa CFFA ambao walionekana kuchoka kufuatia 'moto waliopelekewa' kwenye kipindi cha kwanza.

Ndipo Wananchi wakafanikiwa kuongeza mabao mengine matatu kupitia kwa Albert Kangwanda ambaye kipindi cha kwanza alipoteza nafasi adimu. Mabao mengine yalifungwa na Mudathir Yahya na Maxi Nzengeli.

Ni wazi bado safu ya ushambuliaji ya Yanga inapaswa kuongeza umakini kwani wanapoteza nafasi nyingi leo takribani nafasi nane za wazi kwenye kipindi cha kwanza.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Goals; CFFA 0-4 Yanga (FT)
Goals; CFFA 0-4 Yanga (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Kikosi : CFFA vs Yanga, CAFCL R1
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Matchday; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 17 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 17 2026
11h ago
READ MORE β†’
Diarra hatihati kuikoa CFFA
Diarra hatihati kuikoa CFFA
22h ago
READ MORE β†’
Yanga kusaka rekodi ya kufuzu makundi kwa msimu wa nne mfululizo
Yanga kusaka rekodi ya kufuzu makundi kwa msimu wa nne mfululizo
1d ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka mkazo, hawatawadharau CFFA
Manqoba aweka mkazo, hawatawadharau CFFA
1d ago
READ MORE β†’
CFFA vs Yanga; Tiketi zinaelekea ukingoni, umekata yako?
CFFA vs Yanga; Tiketi zinaelekea ukingoni, umekata yako?
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 16 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 16 2026
1d ago
READ MORE β†’
CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
2d ago
READ MORE β†’