Mlinzi wa Yanga Israel Mwenda leo amejiunga rasmi kikosini baada ya kumalizika kwa sakata lake na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
Mwenda leo amejumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya kikosi cha Wananchi kinachojiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA ambao utapigwa Jumatano, Oktoba 21 uwanja wa Azam Complex.
Hivi karibu uongozi wa Yanga ulithibitisha kumalizana na beki huyo aliyekuwa nje kwa miezi kadhaa baada ya shauri lake kumalizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF.
Urejeo wake ni habari njema kwa Wananchi wakati huu ambao timu inakabiliwa na ratiba ya kucheza mechi mfululizo.

ADVERTISE HERE