Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake

Wakati mashabiki wa Yanga wakiendelea kushuhudia mabadiliko ya kiufundi ya timu yao chini ya kocha Manqoba Mngqithi, kuna aina fulani ya ufundi umeanza kuonekana kwenye eneo la kiungo ambalo anatumika Fred Duval Ngoma.

Raia huyo wa Jamhuri ya Congo Brazzavile, ameanza kuwateka mashabiki wa Yanga kutokana na staili yake ya uchezaji inayochanganya utulivu wa hali ya juu na matumizi makubwa ya akili ya mpira (football brain).

Tofauti na viungo wengi wakabaji wanaosifika kwa rafu na matumizi makubwa ya nguvu, Ngoma yeye ni mchezaji wa aina tofauti kabisa.

Yeye ni mfano halisi wa kiungo wa chini anayepanga mchezo (deep-lying playmaker). Anacheza bila haraka, anajua namna ya kulinda eneo lake mbele ya mabeki, na kila anapopokea mpira chini ya shinikizo la wapinzani, hutumia "first touch" yake tulivu kuanzisha mashambulizi mapya kwa kupiga pasi za uhakika.

Sifa kuu inayomtofautisha Ngoma uwanjani ni uwezo wake mkubwa wa kusoma mchezo mapema (anticipation). Badala ya kukimbia hovyo, anajua kusimama kwenye nafasi sahihi jambo linalomfanya arejeshe miliki ya mpira kwa timu yake (ball recovery) kwa urahisi.

Kocha Mkuu wa Yanga Manqob Mngqithi ameonekana kumtumia Ngoma katika mbinu zake kama kiungo mchezeshaji kutokea chini, njia za mipira inayokwenda mbele mara nyingi huanzia kwake.

Ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi ambazo wakati mwingine zinavuka hadi mistari miwili ya ulinzi.

Moja ya maeneo ambayo kocha Manqoba amebainisha kuimarika kwenye kikosi chake ni uwezo wa kuzifungua timu zinazojiilinda kutokea chini (low block).

Uwepo wa viungo kama Ngoma kwenye kikosi cha Yanga pengine ni moja ya sababu ya mafanikio hayo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
21h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Toure ameweka kambani kila raundi CAFCL
Toure ameweka kambani kila raundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’