Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amekosekana katika mechi mbili zilizopita kutokana na changamoto ya jeraha la mkono.
Mwamnyeto alipata majeraha katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA.
Hata hivyo tayari ameanza kujifua na wachezaji wenzake ikiwa ni hatua nzuri kuelekea kurejea kikosini.


Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa wakati nahodha akikaribia kurejea, nahodha msaidizi Dickson Job amerejea kikamilifu baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.
Kwa mara ya kwanza Job alitumika kwa dakika zote 90 kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa Fc ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
ADVERTISE HERE