Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime

Baada ya mapumziko ya kalenda ya FIGFA, Klabu ya Yanga inakwenda kukabiliana na ratiba ngumu ya mechi mfululizo mwishoni mwa mwaka huu, huku ikilazimika kugawa nguvu zake sawia kati ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na kusaka tiketi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Kundi B.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya NBC, wataanza na Ligi Kuu tarehe 20 Novemba watakaposafiri kuwafuata Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro, kabla ya kuelekea mkoani Mbeya kukipiga na Mbeya City tarehe 27 Novemba mechi ambayo hata hivyo huenda ikapigwa kalenda kutokana na muingiliano wa ratiba na kalenda ya ligi ya mabingwa.

Baada ya hapo, miamba hiyo itarejea jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Azam FC, katika mchezo utakaopigwa Desemba 5 (unaweza kusogezwa mbele), kisha kusafiri tena kuwafuata Singida Black Stars Desemba 12, na kuhitimisha mwaka kwa kurudiiana tena na Azam FC tarehe 30 Desemba.

Wakati mapambano hayo ya ndani yakiendelea, macho na masikio ya mashabiki wa Yanga yatakuwa pia kwenye anga la kimataifa ambapo timu hiyo imepangwa Kundi B la Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na timu za Zamalek SC, MC Alger, na Club Africain.

Ratiba kamili ya Yanga katika hatua hiyo ya makundi imepangwa kama ifuatavyo:

  • Mechi ya 1: Yanga SC vs MC Alger – Jumamosi, 28 Novemba 2026 (Nyumbani) 
  • Mechi ya 2: Club Africain vs Yanga SC – Jumamosi, 5 Desemba 2026 (Ugenini)
  • Mechi ya 3: Zamalek SC vs Yanga SC – Ijumaa, 18 Desemba 2026 (Ugenini)
  • Mechi ya 4: Yanga SC vs Zamalek SC – Ijumaa, 8 Januari 2027 (Nyumbani)
  • Mechi ya 5: MC Alger vs Yanga SC – Ijumaa, 15 Januari 2027 (Ugenini)
  • Mechi ya 6: Yanga SC vs Club Africain – Ijumaa, 22 Januari 2027 (Nyumbani)
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
17h ago
READ MORE β†’
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
1d ago
READ MORE β†’
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
1d ago
READ MORE β†’
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
2d ago
READ MORE β†’
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
2d ago
READ MORE β†’