Yanga Princess yaandikisha ushindi wa pili ugenini WPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Yanga Princess yaandikisha ushindi wa pili ugenini WPL

Kikosi cha Yanga Princess kimeanza vyema kampeni ya ligi kuu ya Wanawake msimu huu (WPL) leo wakiichapa Geita Queens mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa huko Geita.

Mesay 'The Shasha woman' ameendeleza mwanzo mzuri wa kuzifumania nyavu leo akifunga bao lake la pili.

Mesay pia alifunga bao kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bunda Girls katika mchezo wa kwanza uliopigwa Mara.

Mwanzo mzuri kwa kikosi cha Yanga Princess ambacho kinaonyesha kuimarika baada ya kutofanya vyema kwenye michuano ya Ngao ya Jamii.

Kocha Said Maulid 'SMG' na benchi la ufundi wamefanya kazi kubwa kwenye uwanja wa mazoezi kikosi hicho kikiwa mpaka sasa hakijaruhusu bao.

Msimu huu mashabiki wa Yanga wanatamani kuona taji la ligi ya Wanawake linatua Jangwani kwa mara ya kwanza kwenye historia.

Ni msimu wa tano Yanga Princess inashiriki ligi ya Wanawake lakini haijawahi kutwaa ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Alama tisa nyumbani CAFCL ni lazima
Alama tisa nyumbani CAFCL ni lazima
7h ago
READ MORE β†’
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
10h ago
READ MORE β†’
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
1d ago
READ MORE β†’
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
1d ago
READ MORE β†’
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
2d ago
READ MORE β†’